Maisha ya baadaye ya punda nchini Kenya yamegubikwa na giza. Sheria iliyopitishwa na serikali ya Kenya mwaka 1999 ikiidhinisha ulaji wa punda inatishia kuwaangamiza punda wote. Hali hii imechangiwa pakubwa na uwepo wa biashara ya punda nchini Kenya. Biashara hii ni sehemu ya mtandao mkubwa wa biashara ya ngozi ya punda inayoendeshwa na nchi ya Uchina duniani. Nini itakuwa hatima ya punda na wanaomtegemea maishani? Mwanahabari wa Africa Uncensored Kabugi Mbae anatafuta majibu kwenye makala hii.
Add comment